September 3, 2018



Na Mwandishi Wetu, Lagos
MARA ya mwisho tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards maarufu kama (AMVCA) zilifanyika hapa Lagos mwaka 2016 na Tanzania ikatamba zaidi kwa Afrika Mashariki.

Tuzo hizo ni kubwa zaidi kuwatuza watengenezaji wa filamu wakiwemo washika kamera, waigizaji, maprodyuza na kadhalika. Safari hii zimerejea na Wakenya wameonyesha walijipanga.

Wakenya wameshika nafasi ya pili kutawala katika tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards, maarufu kama (AMVCA) zilizomalizika juzi hapa jijini Lagos, Nigeria.

Wakenya wameshinda tuzo sita kati ya nane walizokuwa wakiwania na kuwapiga kumbo Watanzania kwa upande wa Afrika Mashariki kwa kuwa hawakutoka na tuzo yoyote.

Tanzania ilikuwa ikiwania tuzo mbili kupitia Amil Shivji na Lester Millardo ambao hawakufanikiwa kushinda. Maana yake wamerejea nyumbani wakiwa mikono mitupu huku Tanzania ikiambulia patupu.

Wakenya wameshinda tuzo nyingi na kuwa wa pili kufanya vizuri baada ya Nigeria huku wakiandika rekodi ya kuwa nchi ya pili kwa tuzo nyingi kwa wakati mmoja baada ya Nigeria ambayo hutawala kwa kiasi cha asilimia 75 hadi 90 katika tuzo hizo.

Hata Ghana walionekana kushangazwa na kasi ya Kenya ambao wameshinda tuzo hizo sita tena mbele ya Wanigeria na Waghana wenyewe ambao walikuwa wakipewa nafasi kubwa zaidi.

Asilimia kubwa ya Wakenya walioshinda wameonyesha wazi kwamba walipania kubeba tuzo zote nane na waliona kwa tuzo hizo mbili walizozikosa, watakachofanya ni kupambana zaidi ili wapate kuingia katika vipengele vingi zaidi za kugombea tuzo hizo.

Katika Ukumbi wa Hoteli ya Eko zilipofanyika tuzo hizo, Kenya walikuwa gumzo kwa mashabiki na wadau wa filamu ambao hawakutegemea kuwaona wakifanya hayo makubwa.



Wengi wao walieleza walivyopambana kuhakikisha wanafikia hapo huku wakiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri, jambo ambalo liliwavutia wengi.
Baadhi ya Wanigeria wameonyesha kuvutiwa na ari ya Wakenya wakisisitiza kwamba ujio wao unaonyesha una jambo na Wanigeria wanapaswa kufanya vizuri zaidi kwa kuwa kumekuwa na filamu nyingi zenye kiwango bora zikitengenezwa nchini humo.

Ukiangalia katika tuzo walizoshinda, wamewashinda Waghana, Wanigeria, Afrika Kusini wanaosifika kwa utengenezaji filamu. Lakini hata kwa Afrika Mashariki, wamewashinda Watanzania, Waganda na Wanyarwanda  na kuonyesha kweli walijipanga kama walivyoeleza.

Nigeria, kama ilivyo kawaida ndiyo wametawala huku mwanamama, Omotola Jalade-Ekeinde akiibuka na tuzo ya mwigizaji bora upande wa drama.

Mkongwe wa cinematographer, Tunde Kelani kutoka Nigeria amefanya vizuri kwa kutokea na kushinda katika tuzo nyingi zaidi huku mshiriki wa zamani wa Big Brother Nigeria, Bisola Aiyeola akiibuka mwigizaji bora wa Tuzo ya Trail Blazer.

WASHINDI WA TUZO NA VIPENGELE HUSIKA;
Muigizaji Bora wa Komedi
Odunlade Adekola – A Million Baby

Muigizaji Bora Komedi & Vipindi vya TV
Nyce Wanueri – Auntie Boss

Muongozaji Bora Muvi & Tamthilia
Okafor’s Law – Yinka Edward

Mhariri Bora wa Picha
18 Hours – Mark Maina

Mhariri Bora wa Sauti 
Tatu – Kolade Morakinyo and Pius Fatoke

Wimbo Bora wa Muvi & Tamthilia
Tatu – Evelle

Muingizaji Mwenza Bora
Falz – New Money

Muigizaji Mwenza Bora (mwanamke)
Lydia Forson – Isoken

Muigizaji Bora wa Tamthilia
Omotola Jalade Ekeinde – Alter Ego

Muigizaji Bora Tamthilia (mwanaume)
Adjetey Anang – Keteke

Muvi Bora Afrika Magharibi
Isoken – Jade Osiberu

Muigizaji Bora Afrika Mashariki
18 Hours – Phoebe Ruguru

Muvi Bora Kusini mwa Afrika
The Road to Sunrise – Shemu Joyah

Dairekta Bora
Jade Osiberu – Isoken

Muvi Bora
18 Hours – Phoebe Ruguru

Tamthilia Bora
This Is It – Dolapo Adeleke

Muongozaji Bora wa Sanaa
Lotanna – Tunji Afolayan

Mpambaji Bora 
Tatu – Akpe Ododoru and Tunde Akinniyi

Dizaina Bora Muvi & Tamthilia
Hakkunde – Joan Gbefwi



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic