STARS YAONDOKA BILA YONDANI KUMALIZANA NA THE CRANES YA OKWI UGANDA
Kikosi cha Taifa Stars kimeondoka leo Dar es Salaam kuelekea Kampala Uganda kwa ajili ya mchezo wa kufuzu kuelekea AFCOM 2019.
Tanzania itamenyana na Uganda Septemba 8 2018 kwenye Uwanja wa Nambole huko Kampala ili kusaka tiketi ya kucheza mashindano hayo makubwa Afrika.
Stars imeondoka bila beki wake wa kati, Kelvin Yondani ambaye ameachwa kutokana na kupatwa na majeraha ya mguu.
Uganda itakuwa inaikaribisha Stars ambayo ina wachezaji Emmanuel Okwi na Nicolous Wadada ambao wanacheza soka la kulipwa hapa nchini.








Nawatakia kheri timu yetu ya taifa. Ikitokea tumefungwa wala msihudhunike sana ndio mpira ulivyo kufunga, kutoka suluhu au kufungwa, hayo yatakuwa maelezo ya viongozi wetu wa mpira tulionao. Kocha huyu ni kocha kwelikweli. Nasikia Yondani hatakuwepo ameumia. Yote tumwachie Mungu kwani tuna kikosi kipana sana.
ReplyDeleteLinapokuja suala la timu ya Taifa waganda wapo kitimu zaidi na sio suala la mchezaji mmoja mmoja kwa hivyo Taifa Stars wanatakiwa kuwa makini kutoingia kichwa kichwa kwani hata Mohamed Salah alichemsha pale Nabole.
ReplyDelete