September 27, 2018


Gwiji wa soka wa Simba, Abdallah Kibadeni amesema kuwa anaamini Meddie Kagere wa Simba ana nafasi ya kufanya vizuri kuliko Heritier Makambo wa Yanga kwenye mechi ya watani wa jadi Jumapili.

Kwa mujibu wa Championi Jumatano, Kibadeni amesema kuwa anaamini Kagere ana nafasi nzuri ya kufanya vizuri kuliko Makambo kwenye mch­ezo utakapigwa Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

“Tunachoki­tazama kutoka kwa mtu ni nafasi yake, tunaangalia jinsi gani ana uwezo wa kutumia nafasi uwanjani, nafikiri Kagere anaweza kufanya vizuri Jumapili kuliko Makam­bo,” alisema Kibadeni.

Simba na Yanga zinakutana Jumapili ya wiki hii kwenye uwanja wa Taifa jijin Dar es Salaam ambapo mechi hiyo itaanza majira ya saa 11 za jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic