September 27, 2018


Kiungo wa Simba, Jonas Mkude na wenzake, Jumapili watakuwa na kazi ya ziada ya kufanya kutokana na Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kusema viungo wake, Papy Tshishimbi na Feisal Salum ‘Fei Toto’ ndiyo wana nafasi ya kucheza mchezo huo.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Fei Toto na Tshishimbi wamekuwa wakicheza mara kwa mara na kwenye mechi zote nne za Yanga ilizocheza kwenye ligi mpaka sasa, wawili hao wameonekana kucheza kwa kuelewana sana.

Wakati Yanga ikiwatumia viungo hao, kwa upande wa Simba, msimu huu Mkude ndiye amefanikiwa kucheza mechi nyingi kati ya viungo wote wa kati wa timu hiyo akiwemo James Kotei na Claytous Chama.

Kwa mujibu wa Championi Jumatano, Zahera alisema kuwa wachezaji wake hao anawapa nafasi sababu wanaelewa na wana pumzi.

“Feisal na Tshishimbi ni wachezaji wazuri ambao wanaelewana wanapokuwa uwanjani, ni wapambanaji na wana pumzi na kuweza kucheza vyema bila kuchoka na wakifanya mazoezi zaidi basi watakuwa bora kwenye na­fasi zao hizo.

“Nimekuwa nikiwatumia na nitaendelea ku­fanya hivyo hata kwa michezo ijayo sababu wanazimudu vyema nafasi hizo na wanai­endesha timu vizuri bila tatizo lol­ote,” alisema Zahera.

2 COMMENTS:

  1. Kipigo kiko pale pale hakuna fei totos wala Tshishimbi jitayarishe kufungishwa virago

    ReplyDelete
  2. Mkude Simba hakabiki , ila yeye ndiyo mkabaji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic