September 18, 2018


Baada ya kufunga mabao matatu pekee ama hat trick katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, imeelezwa kuwa straika wa Stand United, Alex Kitenge hakupewa mpira wake.

Taarifa imesema kuwa Kitenge aliishia kupiga picha na mpira badala ya kuondoka nao huku ikielezwa kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini lina uhaba wa mipira jambo ambalo limepelekea asikabidhiwe.

Tukio hilo la aina yake limewashangaza wengi na kupigwa na butwaa juu ya TFF kuwa iweje ikose mipira ya kutosha ikiwa kama mama wa soka la Tanzania.

Licha ya kutopewa mpira huo, imeelezwa pia TFF wamemuahidi kumpatia Kitenge mpira wake kwa siku za usoni pale itakapopatikana mingine ili iwe kama kumbukumbu kuwa alifunga hat trick.

Kitenge amekuwa gumzo ikiwa ni siku ya tatu sasa tangu amtungue kipa Mkongo wa Yanga, Klaus Kindoki na kumuachia lawama kwa mashabiki wa timu yake ambao wengi wameutaka uongozi wa Yanga kutomtumia tena.

2 COMMENTS:

  1. Hovyo kabisa wao TFF kazi yao kubwa kutizama mangufu ya wenzao wakati wao mizengwe mitupu.

    ReplyDelete
  2. TFF nao waadhibiwe. Afisa anayeshughulikia kuwepo mipira afungiwe kwa kufanya uzembe na hujuma. Mwaka mmoja na faini shilingi laki 5....... TFF kwisha .......ubabaishaji mtupu. Mnakosaje Mdhamini?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic