TAMKO LA MASOUD DJUMA KUHUSIANA NA MBELGIJI SIMBA
Baada ya kusikosa safari mbili za klabu ya Simba kuelekea mkoani, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Masoud Djuma, amesema kuwa amebakia Dar es Salaam kwa majukumu makubwa mawili, imeelezwa.
Taarifa imeeleza kuwa Djumma amesema hakuweza kuambatana na kikosi cha Simba kuelekea Mtwara pamoja na Mwanza kutokana na kupewa majukumu na Kocha Mkuu, Patrick Aussems ya kuwasoma Yanga wakicheza Taifa.
Djuma alihudhuria mechi ya Yanga jana dhidi ya Coastal Union ili kujua timu hiyo mbinu inazozitumia kuelekea mechi yao ya watani wa jadi Septemba 30 2018.
Mbali na kuwapigia chapuo Yanga, Djuma amesema amesalia Dar es Salaam kuendelea kuwanoa wachezaji ambao hawasafiri na kikosi kwenda Mwanza kucheza na Mbao ili kuwaweka fiti zaidi.
Juuko Murushid pamoja na Haruna Niyonzima, ni baadhi ya wachezaji ambao wapo kwenye program hiyo chini ya Djuma wakijifua kurejesha makali yao baada ya kutokuwa na timu kwa muda mrefu.
Acheni kumlishia maneno Masoud Djuma. Hivyo mtu anaekupeleleza kwa kutafuta usiri wako atatamka hadharani?
ReplyDeleteTime will tell......kwan kuna mech 2 tu muhimu msimu mzima !?
ReplyDeleteSafiii
ReplyDelete