September 20, 2018


Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, jana alitumia dakika 40 pekee kuwaandaa wachezaji wake tayari kwa mtanange wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC leo.

Mbelgiji huyo alitumia dakika hizo kwa ajili ya kuwanoa wachezaji wake namna ya kushambualia na kumalizia uzuri pasi za mwisho.


Aussems hakutaka kuwachosha zaidi wachezaji kwani anajua ugumu wa mechi za mikoani kutokana na changamoto aliyoipata dhidi ya Ndanda FC kwenye mechi iliyopita.

Simba inakutana na Mbao ambayo ina hasira ya kupoteza mechi ya mwisho dhidi ya JKT Tanzania huku wakiumizwa na watani zao wa jadi Yanga ambao wameshinda dhidi ya Coastal Union jana.

Kuelekea mechi hiyo, Simba itazidi kuwakosa baadhi ya wachezaji wake nyota ikiwemo Juuko Murushid na Haruna Niyonzima ambao wamesalia Dar es Salaam kuendelea na program maalum inayoongozwa na Kocha Msaidizi, Masoud Djuma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic