September 27, 2018


Na George Mganga

Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumtangaza Jonesia Rikiyaa kama PILATO atayaechezesha mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga Jumapili ya wiki hii, uongozi wa Simba umesema ni vema akafuata sheria 17 za mchezo wa soka.

Simba wamesema ni haki kwao kumkosoa pale anapokosea na pia kusifia pale inapotokea amefanya vizuri kwa kuchezesha vema bila kuvunja sheria ndani ya dakika 90.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameeleza kuwa wao hawana tatizo na Waamuzi wote waliotangazwa na badala yake wakiomba tu mchezo uchezeshwe kwa haki.

Manara amesema mamuzi ya TFF kuwachagua waamuzi hao yako sahihi na wala hawawezi kuyaingilia kwa maana majukumu yao kama timu ni kucheza mpira na si vingine.

"Hatuwezi kuwaingilia TFF na kuzungumzia zaidi hilo, kifupi tunaomba tu mchezo uchezeshwe kwa haki na kwa kuzingatia sheria 17 za mchezo wa soka bila kuvunjwa" alisema Manara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic