September 27, 2018


Wakati kikosi cha Simba kikiwa katika maandalizi ya moto kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga itakayopigwa Jumapili ya wiki hii, wachezaji wanne wa timu hiyo wameitwa kwenda kuzitumikia timu zao za taifa.

Wachezaji hao ni Juuko Murushid pamoja na Emmanuel Okwi ambao wameitwa kwa ajili ya kujiunga na The Cranes kwa ajili ya kuwania kufuzu fainali za AFCON 2019 dhidi ya Lesotho.

Mbali na Murushid pamoja na Okwi, wachezaji Haruna Niyonzima pia Meddie Kagere nao wameitwa huko Rwanda ili kuanza maandalizi kuelekea mechi na Guinea kusakata tiketi ya kuwania AFCON 2019.

Wakati huo kikosi cha Simba kimezidi kujifua kwenye Uwanja wa Boko Vetrani uliopo pembezo kidogo mwa jiji la Dar es Salaam tayari kuvaana na Yanga wikiendi hii.

Simba watakipiga na Yanga wakiwa wenyeji kwenye Uwanja wa Taifa Septemba 30 2018

1 COMMENTS:

  1. Habari yako iko robo..
    So wameitwa watakosa mchezo wa Jumapili au na wewe pia hujui..??

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic