September 29, 2018


Kuelekea mechi ya Simba na Yanga kesho Septemba 30 2018, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema halitaruhusu mtu yoyote kuwepo nje ya Uwanja huo bila tiketi.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya shirikisho hilo kutangaza zoezi la kuanza kuuzwa kwa tiketi hizo Septemba 20 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wake, Clifford Ndimbo, amesema hakutakuwa na uuzwaji wa tiketi nje ya Uwanja wa Taifa siku ya mechi ili kuepusha vurugu na usumbufu.

Ndimbo ameeleza kwa kesho tiketi zitakuwa zinauzwa chuo cha DUCE pamoja na UHASIBU pekee na si vinginenevyo.

TFF imezidi kuwasisitiza mashabiki na wapenzi wa klabu hizo mbili kuhakikisha wanaenda wakiwa wameshajinunulia tiketi kwa njia ya Selcom ili kuepusha usumbufu baada ya kuwasili uwanjani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic