September 29, 2018


Yanga inaonekana haina presha kuelekea kwenye mchezo wake wa kesho Jumapili dhidi ya Simba, kwani imewatahadharisha wapinzani wao kuwa wasiende na matokeo uwanjani kwani wanaweza kupatwa na hasira kisha wakang’oa viti.

Simba inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mchezo huo namba 72 wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kupigwa kesho Uwanja wa Taifa saa 11:00 jioni huku Jonesia Rukyaa akitara­jiwa kuwa mwamuzi wa kati.

Mwenyekiti wa Kamati ya usajili Yanga, Hussein Nyika alisema huo ni mchezo mkubwa kwa upande wao huku akiwaomba wapinzani wao Simba wasiende na ma­tokeo uwanjani ili kuepusha majanga.

“Ni mchezo mgumu, najua kila timu imejipanga, ila naomba wapinzani wetu wasije na matokeo uwanjani, kitakachotokea pale wakubali na sio waanze kung’oa viti.

“Kama waking’oa viti watakuwa wanaitia hasara serikali yetu kwa sababu zile kodi zetu za wananchi ndiyo zimejenga uwanjani, hivyo waje kupambana tu uwanjani.

“Na pia sisi tumejipanga kupambana, hatuna tatizo lolote na mwamuzi ambaye amepangwa, tunachohitaji ni kujipanga kushinda,” alisema Nyika.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic