September 27, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa Yanga umewataka mashabiki na wadau wa Simba kuacha kuja na matokeo mfukukoni wakiamini kuwa watapata alama tatu katika mchezo utakaozikutanisha timu hizo mbili Septemba 30 2018.

Simba na Yanga zinatarajiwa kushuka dimbani Jumapili ya wiki hii kuendeleza safari ya kuwania kikombe cha Ligi Kuu Bara msimu huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Mashindano Yanga, Hussein Nyika, amesema Simba wanapaswa kuja wakijua kuna ushindani wa hali ya juu tofauti na wanavyodhania kuwa watapata matokeo.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumtangaza Jonesia Rukiyaa kutoka Kagera kama Mwamuzi wa kati atakayechezesha pambano hilo siku hiyo.

Aidha, Nyika ametaka mashabiki wa Simba kutokufanya vurugu uwanjani haswa pale ikitokea wakawafunga ikiwemo suala la kuvunja viti, huku akieleza imekuwa utamaduni wao.

Nyika ameeleza kuwa mashabiki wa timu hiyo wamekuwa wakipaniki pale wanapopoteza dhidi yao na kupelekea kuvunja viti jambo ambalo litaiingizia serikali hasara.

"Nawataka jamaa zetu wasije uwanjani wakiwa na matokeo mfukoni, pia wasije kufanya vurugu maana kwao kuvuna viti ni suala la kawaida" alisema.

3 COMMENTS:

  1. Wewe mwandishi umelogwa nini?waamuzi wenu waliokuws wamekodiwa na manji ndio walisababisha simba kuvunja vitu kutokana na mcheza netball wenu kufunga kinetball zaidi na kukataa baa LA ajibu akidai aliotea wakati sio kweli.sasa mjiaandae kisaikolojia kipigo kiko paleple

    ReplyDelete
  2. MKUMBUSHENI HUYO BWANA KAMA HATA YANGA WAMESHANG'OA VITI

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic