September 27, 2018


Kuelekea mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga, Mashabiki wa wekundu wa Msibambazi, Simba wameibuka na kulitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhakikisha waamzuzi waliopangwa kufuata sheria za mchezo wa soka.

Mashabiki hao wameibuka mara baada ya waamuzi watakochezesha mchezo huo leo kupangwa zikiwa zimesalia siku tatu pekee kabla ya mechi hiyo kupigwa Jumapi ya wiki hii.

Kutokana na mechi hiyo kuwa na msisimko wa aina yake, mashabiki hao wametoa msisitizo haswa kwa Mwamuzi wa kati, Jonesia Rukiyaa wakimtaka afuate sheria zote 17 za mchezo wa soka ili kuepusha balaa ndani ya uwanja.

TFF ilimtangaza jana Mwamuzi Jonesia Rukyaa kuchezesha mechi kati ya Simba na Yanga, Jumapili ijayo Septemba 30 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Rukyaa atasaidiana na Ferdinand Chacha pamoja na Mohamed Mkono na mwamuzi wa Mezani atakuwa Elly Sasii.

1 COMMENTS:

  1. Kwani wewe hutaki mwamuzi afuate sheria 17 za mchezo, na yanga je wao hawataki!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic