September 20, 2018


Wachezaji kadhaa walioachwa wakifanya mazoezi na Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma Jijini Dar es Salaam, huenda wakaikosa mechi dhidi ya Yanga Septemba 30 kama Patrick Aussems akishikilia msimamo wake.

Kocha huyo raia wa Ubelgiji ameiambia Spoti Xtra kwamba; “Nimefurahi kuwaona wachezaji Niyonzima Haruna na Juuko Murshid ni wachezaji niliokuwa nawasikia.

"Kama unavyofahamu hao ni wachezaji wapya kwangu na ukiangalia tayari nina wachezaji niliokuwa nao muda mrefu katika timu ambao tayari wamezoea na kuushika mfumo wangu" alisema.

“Hivyo, ninahitaji muda wa wiki tatu kwa ajili ya kuwaangalia na kuwaingiza katika mfumo mpya ninaoutumia, hivyo siyo kazi kuushika mfumo inahitaji muda kuuelewa,”alisema Aussems ambaye timu yake inacheza na Mbao leo Mwanza.

Wachezaji wengine walioachwa na Masoud ni pamoja na Asante Kwasi, Hassan Dilunga, Said Nduda na Muzamiru Yasin.

2 COMMENTS:

  1. Hiyo siyo sababu , hao ni wachezaji wa kimataifa . mfumo kwa mchezaji ni siku mbili tu na hata masaa mawili . Uongozi umshauri kocha , wasimuachie yeye kila kitu kuamua . simba sasa ni kampuni

    ReplyDelete
  2. Kocha ndie muamuzi wa mwisho katika upangaji wa kikosi msianze mambo ya liswahili na ndio maana Mkongo wa Yanga alimpanga tena kidoki ili kuthibitisha kuwa kocha ndie mwenye jukumu la kupanga nani acheze na nani asicheze sio kufuata mihemko ya mashabiki.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic