September 20, 2018


Kiungo wa kati wa Chelsea raia wa Brazil Willian, 30, anasema hakuwa na mpango wa kuondoka stamford Bridge msimu huu licha ya vilabu vya Manchester United na Barcelona kuonyesha dalili ya kumsaini. (Express)

Mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 20, anapata mafunzo zaidi kutoka kwa mchezaji mwenzake wa Manchester United Romelu Lukaku.

Meneja wa England Gareth Southgate amemtuma naibu wake Steve Holland kumtazama Jack Grealish wakati wa ushindi wa Aston Villa dhidi ya Rotherham siku ya Jumanne wakati anafikiria kumsaini kiungo huyo wa kati wa umri wa miaka 23. (Birmingham Mail)

Mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 33, anasema itakuwa vigumu kwa mtoto wake wa umri wa miaka nane ambaye pia anaitwa Cristiano kucheza mpira kama yeye. Ronaldo Junior anaichezea Juventus Academy. (BeIn Sports, via Sun)

Totttenham wametupilia mbali madai kuwa uwanja wao mpya hautakuwa tayari ifakapo mwanzo wa mwaka 2019. (Sky Sports)


Mkuu mpya wa kandanda huko Arsenal Raul Sanllehi, anataka kumsaini wing'a raia wa Argentina Cristian Pavon, 22, kutoka Boca Juniors. (Football London)

Beki wa Manchester City Aymeric Laporte, 24, anasema ataendelea kuwepo kuichezea Ufaransa licha ya ripoti kuwa huenda anageuza uzalendo wake kwa Uhisania. (Manchester Evening News)


Mshambualiaji wa Liverpool Sadio Mane, 26, amemshauri Roberto Firmino kucheza dhidi ya Paris St-Germain licha ya jeraha lake la jicho.

Mshambuliaji huyo wa Brazil ambaye pia ana miaka 26 alitoka nje na kufunga bao la ushindi siku ya Jumanne. (Liverpool Echo)


Kiungo wa kati wa England James Milner, 32, anasema alipigwa marufuku ya kuvaa nguo nyekundu akiwa mtoto kwa sababu baba yake alikuwa anaichukia Manchester United. (FourFourTwo)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic