September 24, 2018


Mke wa Abdi Banda ambaye ni dada wa Staa wa Bongo Fleva, Alikiba, Zabibu Kiba amefunguka baada ya kumshuhudia mumewe huyo akisakata kabumbu wakati timu yake ya Baroka F.C inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini, ilipoingia dimbani wikiendi iliyopita kumenyana na Orlando Pirates.

ZABIBU amesema alichokiona kwa mumewe huyo akiwa uwanjani ni kwamba ana nidhamu ya mchezo jambo ambalo ni nguzo kubwa ya mafanikio ya mchezaji yeyote mwenye ndoto za kufika mbali zaidi.

Aidha, Zabibu amefunguka kuwa tofauti ya Viwanja vya Tanzania na Afrika Kusini, madhari kwani Sauzi mandhari yake yanavutia zaidi.

Katika mechi hiyo, Orlando Pirates inayoongoza Ligi Kuu ya nchini humo wakiwa na pointi 14 iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Baroka FC wanaoshika nafasi ya 15 wakiwa na pointi 5.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic