October 9, 2018


Baba mzazi wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma amefunguka kwa lugha ya kuchanganya maneno ya Kingereza na Kiswahili kwa kusema; ‘I wish ningekuwepo’ akimaanisha kwamba alitamani kuwepo kwenye sherehe ya kuzaliwa ya mwanaye iliyofanyika Ijumaa iliyopita Uwanja wa Maguniani- Tandale jijini Dar.

Mzazi huyo alisema anatamani angekuwepo kama sehemu ya kukumbuka maisha yao waliyoyapitia miaka ya nyuma akiwa na mwanaye huyo kwani historia aliyoitoa Diamond ilimgusa.

“I wish na mimi ningekuwepo pale. Nilitamani kushuhudia pia mambo mazuri aliyoyafanya mwanangu maana awali nilidhani ni jambo dogo, lakini baadaye nikaona ni jambo kubwa sana.

“Nilipofuatilia kwenye TV nikaona mwanangu anatoa Bajaj, anatoa bima, anatoa mikopo kwa akina mama, pamoja na bodaboda kwa kweli moyo wangu ulifurahi sana,” alisema baba Diamond na kuongeza:

“Ile ishu ya kuuza mitumba aliyoizungumza, hata mimi niliuza. Pengine pia ningeweza na mimi kuwatia moyo mamia ya watu waliofurika pale.”

Mzazi huyo alisema, anaamini Diamond alipitiwa tu siku hiyo kumualika kwani anaamini siku hizi hana tatizo naye na wanaongea vizuri hivyo siku nyingine anaweza akamualika.

“Nilisikia alisema amepanga kufanya kila mwaka hivyo bado naamini Mungu akitujalia uzima, ishallah mwakani anaweza kunialika kwani hakuna tatizo kati yetu,” alisema mzazi huyo.

Baba na mama Diamond, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ walitengana miaka mingi iliyopita na kila mmoja akafanya maisha yake na sehemu kubwa ya malezi, Diamond amelelewa na mama yake hadi kupata mafanikio aliyonayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic