HII NDIYO SABABU YA YANGA KUWA JUU DHIDI YA SIMBA HIVI SASA
Kwa matokeo ambayo Yanga inaendelea kuyapata katika mechi zake za Ligi Kuu Bara, ni sahihi kabisa kuwaita ‘baba lao’. Jana baada ya kuwachapa Mbao FC bao 2-0, sasa Yanga imeshinda mechi tano kati ya sita ilizocheza.
Mechi pekee ambayo Yanga haijapata ushindi msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara ni dhidi ya watani wao wa jadi, Simba ambayo ilimalizika kwa suluhu wiki moja iliyopita.
Lakini Yanga ipo mbele ya wapinzani wao hao Simba kwenye msimamo wa ligi, licha ya Wekundu kucheza mchezo mmoja zaidi. Yanga ina pointi 16, wakati Simba wana pointi 14.
Kama Yanga wakishinda mchezo wao mmoja wa kiporo, maana yake watakuwa wameiacha Simba kwa tofauti ya pointi tano.
Yanga ilifanikiwa kupata bao dakika ya 16 likifungwa na kiungo fundi, Raphael Daudi aliyemalizia kwa kichwa faulo iliyopigwa na Ibrahim Ajibu.
Sasa Ajibu amefikisha jumla ya asisti sita katika mechi sita za ligi kuu ambazo Yanga imecheza. Heritier Makambo wa Yanga alikosa bao dakika ya 22 baada ya shuti lake la karibu kabisa na lango kudakwa na kipa wa Mbao.
Kipa Beno Kakolanya kwa mara nyingine alionyesha ubora baada ya kuokoa michomo kadhaa ya wachezaji wa Mbao, hasa dakika ya 22 ilipotokea piga nikupige kwenye lango lake lakini zote akaokoa.
Dakika ya 24, Pastory Athanas alipiga shuti kali akiwa nje ya eneo la hatari lakini mpira ukaishia mikononi mwa Kakolanya.
Mbao walionyesha kandanda safi katika mchezo huo lakini walishindwa kuzitumia vizuri nafasi walizotengeneza.
Pastory alionekana kuwa mwiba mkali zaidi kwa mabeki wa Yanga na walilazimika kumchezea faulo za mara kwa mara ili kumpunguzia kasi. Kakolanya alitoka dakika ya 59 baada ya kuumia na kubebwa kwenye machela hadi vyumbani, na nafasi yake ilichukuliwa na Klaus Kindoki.
Ajibu alipiga bao la pili la Yanga dk ya 92 kwa tik tak safi ambapo mpira uligonga mwamba wa juu na kuzama wavuni. Yanga: Beno Kakolanya/ Klaus Kindoki dk ya 54, Paul Nyanganya, Gadiel Michael, Andrew Vicent/ Abdallah Shaibu ‘Ninja’ dk ya 74, Kelvin Yondani, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Deus Kaseke, Raphael Daudi, Heritier Makambo, Ibrahim Ajibu na Matheo Anthony/Thaban Kamusoko dk 53.
Matokeo ya mechi nyingine, Biashara United ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Karume mjini Musoma, ilichapwa 0-2 na Mwadui FC shukurani kwa mabao ya Ibrahim Nasser (65) na Lameck Chamkaga aliyejifunga dk ya 89.
JKT Tanzania ikiwa nyumbani ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Alliance. Abdulrahman Mussa aliifungia JKT (70) huku Juhudi Philimon akiifungia Alliance dk ya 90.
Kumbuka tangu ligi ianze Yanga hajatoka nje ya Daresalam? Simba ilishapoteza mechi yeyote aliyocheza Daresalam? Hapana. sasa hizo sifa za kijinga anazopewa Yanga zinatoka wapi?
ReplyDeletehawa waandishi bila kuitaja simba kwa mabaya hawajisikii baada ya mechi tano watakuwa kimya kwani msimamo wa ligi utakuwa umebadirika
Deletesisi yanga tunapiga nje ndani . hatuangalii viwanja . tutaenda mikoani na tutachukua point zetu
ReplyDeletehivi hujui kuwa hadi sasa Yanga wanacheza nyumbani tu? Azam na Simba wameteleza mecha za ugenini.Tutajua Yanga ni zaidi ya Simba au Azam pale watakapoanza kucheza mechs za ugenini? Hata msimu uliopita Yanga walianza kuwa wanafungwa mfululizo kwenye mechi za ugenini.Wakaanza mbeya, singida na kwa mtibwa kote wanafungwa tu
ReplyDeletewewe mwandishi ni mpuuzi..hivi kwa akili yako finyu ya kufikiria uhalisia yanga ingemfunga Mbao magoli mawili Mwanza
ReplyDeleteSio kosa lako jipange mechi za ugenini utajuta wewe,huwajui Mbao au umewasahau,kuna azam kuna jkt Tanzania kuna coast union hizi mechi zote ukijitahidi sana labda sare,utapigwa tu hata ufanye nn.
ReplyDeleteYanga kachukua ubingwa Mara 27 hakukuwa na mechi za Minoan?endeleen kuxubilia embe chini ya mnazi
ReplyDeleteSimba na yanga nani mwenye vikombe vingi
DeleteMbona mapovu wanaz Wa simba !?
ReplyDeleteKwann washabiki wa simba mnakua wakal Sana mbona mkizungumziwa nyinyi meno nje mlijiunga bando kusoma habar za simba tu???πππππ
ReplyDeleteHii blog igeuzwe iwe ya Yanga.Ingekuwa Azam au Simba kucheza mechi za DΓ€r tu ingekuwa tatizo.Tungeambiwa ohh ngoja waende mikoani.Msimu uliopita Okwi alikuwa anafunga Dar ikaanza witchhunt. Leo Yanga imecheza Dar tu hamna comment za waandishi.Kocha wao deiwaka kwani pia ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Kongo. Hamna timu yeyote kubwa inayofundishwa na kocha deiwaka huku akiwa na timu nyingine. Ingekuwa ni Simba vingeandikwa vitabu wacha makala kwenye magazeti.Ligi bado mbichi.
ReplyDeleteKwa kiwango cha Yanga sidhani kama watashinda kwenye viwanja vigumu kama Nangwanda, Kirumba, Sokoine na hata ule wa Kambarage. Time will tell.
ReplyDeleteEwe Sutta,hakuna kiwanja cha ugenini kwa simba na Yanga hapa Tanzania kwani kila wanapokwenda kucheza wao ndio wanakuwa wengi uwanjani na hata kumiliki mji na uwanja ni vyao.Simba kapigwa kwavile hawezi kucheza mechi za ugenini tofauti na Yanga yenye wachezaji wengi wa uswahulini.
DeleteWambura pia amesema kwamba Simba imepigwa faini ya Sh. 500,000 kutokana na mashabiki wake kuwarushia chupa za maji na soda viongozi, wachezaji na kocha wao Mkuu, Mbelgiji Patrick J. Aussems baada ya mechi namba 48 dhidi ya Mbao FC walioshinda 1-0 Septemba 20 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza kumalizika. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.
ReplyDeleteKWa hali hiyo unataka Simba ishinde mkoani,imshinde nani labda Simba b
nauliza tu hivi wachezaji wa nje wanaoruhusiwa kusajiliwa na vilabu ni saba (7) au tisa (9) maana naona Simba wamesajili wachezaji tisa (9) !!!!!
ReplyDeleteNi kumi unasajili kulingana na uwezo wako...Simba watamleta rasta wa asante kotoko ili ikamilishe
DeleteHata mbao au mtibwa sugar wrote wanafanya vizuri wakicheza nyumbani..ushindi wa Yanga sio mkubwa kivile hawajaizidi hata timu moja zaidi ya bao tatu...sana sana ni moja au mbili..so huwezi kusema Yanga ni wazuri!
ReplyDeleteUjatoa sababu ya maana huwezi kuipima timu kwa mechi tano.
ReplyDeleteMpuuzi....hujataja sababu hapo juu
ReplyDelete