October 22, 2018






NA SALEH ALLY
UKISEMA ni jambo zuri linalopaswa kusindikizwa na dua za kumshukuru Mungu, ninaamini nitakuwa nimepatia sana.

Nikiwa jijini Johannesburg wakati nikitafuta taxi inipeleke sehemu, nilishangazwa na mfanyakazi wa hoteli niliyofikia akitaka kujua kuhusiana na Mo Dewji.

Hii ilikuwa bado hajapatikana, siku ambayo IGP, Simon Sirro alipoonyesha picha ya gari ambalo lilitumika kufanya utekaji huo.

Nilijaribu kumuelezea na ilionekana alikuwa akisikia vitu vingi ambavyo havikuwa na ukweli. Lakini nilipokuwa kwenye taxi, njiani dereva aligundua natokea Tanzania baada ya kusikia nazungumza Kiswahili.

Yule dereva naye akaanza kuniuliza kuhusiana na suala hilohilo, kwa kweli lilinishangaza sana. Maana yake limekuwa ni jambo kubwa ambalo linatafsiriwa kwa kila aina ya maana.

Maana yake hakuna asiyejua kuhusiana na kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji ambaye hakuonekana kwa siku tisa.

Dewji maarufu kama MO, hakujulikana alipo hadi alipoipigia simu familia yake na kueleza alipo wamfuate.

Mo alitekwa na watu wasiojulukana Oktoba 11 wakati akiingia gym katika Hoteli ya Colloseum jijini Dar es Salaam.

Kulikuwa na mengi kuhusiana na kupotea kwake na wakati mwingine ukisikiliza kila jambo unaweza kuchanganyikiwa, maana unasikia hili mara lile, hapa mara kule.

Linapotokea jambo kama hili kila mmoja anakuwa na aina yake ya anavyopokea, anavyochukulia na kadhalika. Lakini kikubwa kabisa ambacho Watanzania wote waliomba ni Mo Dewji kurudi salama.

Mungu ameliwezesha hilo kwa kuwa ndiyo muhimu zaidi. Uhai wake ni jambo namba moja kwake, familia yake lakini pia wanafamilia wake kwa maana ya ndugu jamaa na marafiki.
Ambacho nakiona baada ya kurejea kwa Mo kikubwa sasa ni suala la kufurahia maisha naye pamoja badala ya kuyakuza na kufanya mambo ambayo si sahihi.
Si sahihi kuendelea kulalama, kulumbana, kuzusha, kuhisi na kadhalika. Badala yake tumshukuru Mungu na kuendelea na maisha yetu ya kawaida.
Tumfanye Mo aamini amerejea nyumbani, yuko na anaweza kuendelea na maisha yake ya kawaida. Kuendelea kulaumu, kulaumiana, kushambuliana mwisho tutaingia kwenye malumbano yasiyokuwa na sababu.

Ninaamini vyombo vya usalama vitashughulika na waliohusika kama walivyoahidi. Sisi tuendelee na maisha tukiwa pamoja na Mo ambaye amerejea salama.

Tunaamini naye atakuwa kwenye utulivu wa hali ya juu na kuendelea na mambo yake kama kawaida.




2 COMMENTS:

  1. Unaongea ungwege gani tusipo komesha hii ali mtakomesha lin au mpaka atekwe mwingine afe ndoo watu waongee acha ujinga tuna haki ya kujaji kilicho tokea maana sio mara ya kwanza achen uduanzi

    ReplyDelete
  2. unachoandika sio fani yako, baki kule ulikozoea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic