Mshambuliaji wa Simba, Adam Salamba leo alikuwa ndani ya kikosi kilichocheza dhidi ya Ruvu Shooting, amesema kuwa uwezo wa Meddie Kagere, John Bocco na Emanuel Okwi ndani ya Simba unamfanya aongeze juhudi ili aweze kupata nafasi .
Salamba amefikisha mabao 2 msimu huu baada ya leo kufunga bao la tano akitokea benchi dakika ya 82 akichukua nafasi ya Emmanuel Okwi ambaye alipata majeraha, amesema kuwa anapata tabu kupata namba.
"Simba inawachezaji wengi ambao wana uwezo mkubwa kuna ugumu wa kupata namba ya kudumu hivyo kila nikipata nafasi ni lazima nipambane kuhakikisha naisaidia timu yangu kupata matokeo nitafanya kila wakati ninapopata nafasi," alisema.
Simba wamefanikiwa kushinda mchezo wake wa 7 baada ya kucheza michezo 10 wamepoteza mchezo mmoja na kutoa sare michezo miwili wamefikisha jumla ya pointi 23 na wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo na Azam wakiwa vinara baada ya kufikisha pointi 27.
0 COMMENTS:
Post a Comment