October 30, 2018



Kutokana na kukosa nafasi ya kusugua benchi wala kucheza beki wa kati wa timu ya Simba, Yusuf Mlipili ameamua kujiondoa katika timu hiyo.

Mlipili alijiunga na Simba msimu uliopita akitokea timu ya Toto Africans ya jijini Mwanza, anadaiwa kutimka zake katika kikosi hicho yapata wiki sasa.

Habari kutoka ndani ya Simba ziliezleza kuwa baada ya kuona hana nafasi ndani ya kikosi cha timu msimu huu tofauti na msimu uliopita ambao alikuwa yupo kikosi cha kwanza.

"Hata viongozi hawajui alipo kwa sababu kaondoka bila kutoa taarifa na sasa yapata wiki, mazoezi yote tuliyofanya ya kujiandaa dhidi ya Alliance FC, Stand United pamoja na Ruvu Shooting hakuwepo," kilieleza.

Kocha Mkuu Patrick Aussems alisema kuwa hana taarifa zake hivyo hawezi kumzunguzia mchezaji huyo.

4 COMMENTS:

  1. kama ni kweli basi atakua anajipoteza mwnyw, coz mwaka jana kamuweka benchi Juuko, Bukaba hata Nyoni alikua anasubiri kwake, iweje yy asiwe mvumilivu!

    ReplyDelete
  2. Huu ndio uzuzu wa wachezaji wa kitanzania, leo hii ulitegemea Mohamed Hussein (Tshabalala) angeingia kikosi cha kwanza Simba?

    ReplyDelete
  3. anashindwa kujituma hawa ndio wachezaji wa masoud juma kwa mzungu anakupanga kwa kiwango

    ReplyDelete
  4. Mlipili alipaswa kupambana na hali yake , mbona wachezaji hawa 8 Mkude , chama,kotei,mzamiru, chama, ndemla, Niyonzima na Dilunga wanapigania nafasi mbili tu na hawajakata tamaa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic