Uongozi wa Yanga umesema kuwa umejipanga kiasi cha kutosha, kuweza kushinda mchezo wao wa leo dhidi ya Lipuli katika mchezo utakaochezwa uwanja wa Taifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hussen Nyika amesema kuwa hawana wasiwasi na kukosekana kwa wachezaji wa timu hiyo ambao ni Ibrahim Ajibu, Papy Tshishimbi na Juma Mahadhiambao ni majeruhi kwa kuwa mbadala wao upo.
"Tuna wachezaji wengi ndani ya kikosi ambao wana uwezo wa kupambana na kupata matokeo kama ambavyo mchezo uliopita hatukuwa na wachezaji wetu Ajibu (Ibrahim), Tshishimbi (Papy) dhidi ya KMC ila tulipata matokeo" alisema.
Taarifa kutoka ndani ya Yanga zilieleza kuwa Ajibu na Tshishimbi wapo fiti kinachosubiriwa ni ruhusa ya daktari ili waweze kucheza ama la.
Kila lakheri majembe yangu,mupone haraka.
ReplyDelete