Kocha mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa kabla ya kumuona Juuko Murshid uwanjani alikuwa anajivunia uwepo wa pacha ya Erasto Nyoni na Pascal Wawa ,uwezo wa Juuko umemshtua.
Kukosekana kwa Nyoni kulimfanya Aussems afanye kazi ya kutengeneza pacha mpya ya Wawa na Murshid jambo ambalo lilikuwa linampa ugumu kutokana na kushindwa kuelewa namna ya kuwatumia.
"Nimejaribu pacha ya Nyoni na Murshid mazoezini na nimeona jinsi inavyocheza vizuri nataka niweze kuwaona wakiwa uwanjani pamoja kwa kuwa bado katika hilo sijafanikiwa .
"Nyoni akimaliza adhabu yake ipo siku nitawaanzisha pamoja ili niweze kujua baada ya hapo pacha ipi itakuwa inastahili katika kikosi changu cha kwanza," alisema.
Nyoni alipata adhabu na shirikisho la soka (TFF) baada ya kudaiwa kucheza mchezo usio wa kiungwana katika mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga hali iliyopelekea kufungiwa michezo mitatu.
Nyoni akipewa dimba la chini mechi vs Azam, patachimbika, aliwatuliza saaana Capeverde!
ReplyDeleteSanaaaaa,ila juuko watasubr sana mafoward wajanja wajanja
Delete