October 4, 2018


Straika wa zamani wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa amezua gumzo la aina yake kwa mashabiki wa Yanga baada ya kuonekana amevalia jezi ya Azam FC na kuamini kwamba atajiunga na timu hiyo kwenye dirisha dogo ingawa Kocha Hans Pluijm amezuga.

Pluijm amesema hajui chochote kuhusiana na picha hiyo ya mchezaji huyo, huku akidai labda imetengenezwa kwenye mitandao ya kijamii lakini Meneja wa Azam, Philipo Alando pia ametamka kitu.

Chirwa kwa sasa anaitumikia Nogotoon ya Misri, ikiwa ni siku chache tu baada ya kuachana na Yanga, aliyoitumikia kwa misimu miwili mfululizo lakini licha ya kwamba amekuwa mgumu kufafanua lakini inaonekana maisha ya Misri siyo kiviile.

“Najua mkataba mpya wa Chirwa huko Misri unafikia mwisho mwezi wa saba mwaka kesho hivyo ni vigumu sana sisi kufanya nae maongezi labda kocha ambaye ni rafiki yake wa karibu,” alisema Alando ingawa kuna kila dalili Chirwa akaja Azam.

LIPULI FC katika mechi saba ambazo imecheza imejikuta ikifunga mabao matatu na kufugwa matatu, hii ni kwenye ligi kuu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic