ZAHERA, STAM WABEBA TUZO ZA UKOCHA BORA LIGI KUU
Kamati ya Tuzo za Wachezaji Bora Ligi Kuu Tanzania Bara, imeanzisha tuzo mpya ya Kocha Bora wa mwezi itakayokuwa inatolewa kila mwezi kwa lengo la kutambua mchango wa kocha husika katika ligi hiyo.
Baada ya kamati kukaa chini na kuanzisha tuzo hizo, ya kwanza imefanikiwa kwenda kwa Kocha wa Mbao, Amri Said akiwa kama Kocha bora wa mwezi Agosti.
Vilevile Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, ametwaa tuzo hiyo akiwa kama Kocha bora wa mwezi Septemba.
Tuzo hizo ni chachu kwa makocha wote wa Ligi Kuu Bara kama changamoto ya kuhakikisha klabu zao zinafanya vizuri ili kujitengenezea mazingira ya kuwa washindi kila mwezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment