October 10, 2018

OMOG



Unaweza kusema kashangaa! Maana baada ya juzi Jumatatu uongozi wa Simba, kuthibitisha kuachana rasmi na aliyekuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Mrundi, Masoud Djuma, kocha wa zamani wa kikosi hicho, Mcameroon, Joseph Omog ameibuka na kusema kuwa ameshangazwa na uamuzi huo kwa kuwa haukuwa wa busara.

Simba imefikia uamuzi huo kufuatia madai ya kutokuwepo maelewano kati ya Djuma na kocha mkuu, Mbelgiji, Patrick Aussems.

Omog alisema kuwa kwa upande wake anaona Simba imefanya maamuzi ya kushangaza kwa kuamini jambo waliloambiwa na upande mmoja bila ya kuangalia umuhimu wa mtu waliyemuondoa.

“Binafsi naona ni jambo la kushangaza, Simba wamemfukuza Djuma, tatizo lilikuwa nini mpaka wamechukua maamuzi hayo, kwangu Djuma alikuwa ni  kama mtoto wangu ninayemlea na wala hatujawahi kukosana kwenye kazi, wakati mwingine kupishana mawazo ni kawaida lakini ninachokisikia kipo tofauti sana.

“Kwangu naona bado Simba ilikuwa inamuhitaji kwa kuwa ameshakaa nao na anajua kila kitu, sasa kwa hali hiyo sioni nafasi ya wao kufika mbali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kuwa huyo mwalimu nimesikia tu ametoka Ubelgiji, simjui kabisa,” alisema Omog.

Ikumbukwe, Omog alifanya kazi na Djuma kwa kipindi kifupi kabla ya Mcameroon huyo kutimuliwa mwishoni mwa mwaka jana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic