Nonga amesema kuwa walikuwa wana uwezo wa kufunga ila wamekosea kosa moja ambalo wapinzani wao wametumia nafasi hiyo waliyoipata.
"Tumecheza mpira tumejituma, tumeshindwa kutumia nafasi ambazo tumezipata kutokana na kupoteza umakini hasa kwa nafasi ambazo tumezitumia, tumeona makosa yetu tutafanya vizuri mechi zetu zijazo," alisema.
Lipuli wamepoteza mchezo wao mbele ya Yanga baada ya kushinda mchezo wao uliopita dhidi ya Mbao hali iliyowafanya wajiamini kuwa wanaweza kupata matokeo kwa kufungwa bao 1-0.
wow this is a good content. thanks sports news
ReplyDelete