Kadi aliyopata mchezaji wa timu ya Yanga, Paul Godfrey imemliza kutokana na kuwa na mipango mingi ya kufanya kuisaidia timu yake, ila kwa kuwa imetokea ameipokea adhabu hiyo.
Paulo alipata kadi hiyo katika mchezo dhidi ya Lipuli uliochezwa jana Uwanja wa taifa na wakaibuka na ushindi wa bao 1-0, baada ya kumchezea rafu Miraji Adam dakika ya 84 aliyekuwa anaambaa na mpira kuelekea maeneo ya Beno Kakolanya.
"Ni sehemu ya mchezo hivyo najipanga kwa ajili ya michezo mingine kikubwa tumepata matokeo tumemaliza salama hilo ni jambo la msingi kwetu," alisema.
Paul ameaminiwa na kocha Mwinyi Zahera baada ya kupandishwa kikosi B na kufanikiwa kuonyesha uwezo wake ambao umemfanya aweze kupata namba kikosi cha kwanza .
Wachezaji wa Yanga wanaonekana kutumia zaidi nafasi wanapochezeshwa na Ajibu hivyo kocha anatakiwa kumtengeneza mchezaji mwingine kama alivyomtengeneza Ajibu ili asaidie yaani awe mbadala wa Ajibu,hilo liko wazi yanga wanaelewa zaidi staili ya pasi za ajibu na kupata matokeo matamu
ReplyDeleteFei toto akichezeshwa mbele anaweza shida ana
ReplyDeleteWatakoma na hawana kikosi kipana!
ReplyDelete