October 30, 2018



Kiungo mkabaji wa timu ya Yanga Feisal Salim 'Fei Toto' amesema kuwa ushindi walioupata umetokana na umakini wa wachezaji hasa kwa kufuata maelekezo ya mwalimu.


Fei Toto alikuwa ndani ya kikosi ambacho kimeivaa Lipuli inayonolewa na Selemani Matola, leo na kufanikiwa kushinda kwa bao 1-0 katika uwanja wa Taifa, lilifungwa na Herietier Makambo dakika ya tisa.


"Namshukuru Mungu tumemaliza mchezo salama, kikubwa ni umakini wa wachezaji hasa katika kufuata maelekezo ya mwalimu hali ambayo imetupa matokeo," alisema.


Yanga wamecheza michezo 9 yote wakitumia Uwanja wa Taifa, wamefanikiwa kuchukua pointi tatu kwenye michezo nane na kutoa sare mchezo mmoja, wamefikisha pointi 25 huku vinara Azam wakiwa na pointi 27 baada ya kucheza michezo 11.

6 COMMENTS:

  1. Wachezaji wa Yanga wanaonekana kutumia zaidi nafasi wanapochezehwa na ajibu hivyo kocha anatakiwa kumtengeneza mchezaji mwingine kama alivyomtengeneza ajibu ili asaidie yaani awe mbadala wa Ajibu,hio liko wazi yanga wanaelewa zaidi staili ya pasi za ajibu na kupata matamu zaidi!

    ReplyDelete
  2. Wachezaji wa Yanga wanaonekana kutumia zaidi nafasi wanapochezeshwa na Ajibu hivyo kocha anatakiwa kumtengeneza mchezaji mwingine kama alivyomtengeneza Ajibu ili asaidie yaani awe mbadaa wa Ajibu,hilo liko wazi yanga wanaelewa zaidi staili ya pasi za ajibu na kupata matokeo matamu

    ReplyDelete
  3. Wachezaji wa Yanga wanaonekana kutumia zaidi nafasi wanapochezeshwa na Ajibu hivyo kocha anatakiwa kumtengeneza mchezaji mwingine kama alivyomtengeneza Ajibu ili asaidie yaani awe mbadaa wa Ajibu,hilo liko wazi yanga wanaelewa zaidi staili ya pasi za ajibu na kupata matokeo matamu

    ReplyDelete
  4. Wachezaji wa Yanga wanaonekana kutumia zaidi nafasi wanapochezehwa na ajibu hivyo kocha anatakiwa kumtengeneza mchezaji mwingine kama alivyomtengeneza ajibu ili asaidie yaani awe mbadala wa Ajibu,hio liko wazi yanga wanaelewa zaidi staili ya pasi za ajibu na kupata matamu zaidi!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic