October 14, 2018


Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Kangi Lugola amewaambia waandishi wa habari jana Jumamosi jijini Dar es Salaam kwamba bado wanaendelea na upelelezi wa kina wa kutekwa kwa mwanachama huyo mtiifu wa Simba. 

Aliongeza pia katika upelelezi wao wanawashikilia watu 20 kwa uchunguzi na akaamuru kwamba kama kuna ambaye watajiridhisha kuwa hana hatia aachiwe arudi uraiani ndani ya saa 24.

Alisisitiza kuwa katika watu wanaowashikilia kuhusiana na sakata hilo hawezi kuwaweka wazi kwa
vile atavuruga upelelezi. “Zipo sababu nyingi ambazo zinapelekea mtu kutekwa.

Zingine ni za kisiasa, kiuchumi, ushirikina, mapenzi, visasi na kudhulumiana,”alisema Lugola ambaye ni mpelelezi aliyebobea. 

“Kiuchumi inaweza kuwa watu wana njaa wanaona wakimteka mtu mwingine watapewa kiasi fulani cha fedha kwa vile ana hela,”alisema Kangi mwenye miaka 55. 


Alisisitiza kwamba kwenye ishu ya MO na zingine zinazohusiana na utekaji taarifa rasmi itatolewa na jeshi la polisi na si watu wengine.

Kangi alisema kwamba polisi wanaendelea kumtafuta MO popote alipo ingawa hakuwa tayari kuweka wazi kama uchunguzi wao umebaini bado yupo ndani ya ardhi ya Dar es Salaam au la.

CHANZO: SPOTI XTRA

4 COMMENTS:

  1. Utekwaji wake unaviashiria vyote vya vitendo vya kigaidi na uvunjifu wa amani,na wasiwasi wa watanzania kujihisi kuwa hawapo huru ndani ya nchi yao na mali zao ni mkubwa mno kuliko wakati wote ule tangu nchi yetu kupata uhuru baada ya hili tukio. Yakujiuliza kwanini Jeshi la wananchi lisishirikishwe katika msako wa kumtafuta Mo pengine wana vitu vya ziada.

    ReplyDelete
  2. Wenye dhamana ya upelelezi ni Police lakini huwezi jua inawezekana serikali imeshashirikisha vyombo vyote vya usalama ila inakuwa ni siri.

    ReplyDelete
  3. jeshi la wananchi haliwezi kuhusishwa kwa sababu ya mgawanyo wa kazi ingawa wanaweza kuhusishwa kuhakikisha hatoki nje ya mipaka ya Tanzania hiyo ndio kazi yao kuu hapa ni polisi na usalama wa Taifa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic