Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amebainisha kinachompoza mshambuliaji Herieter Makambo kwa kucheza chini ya kiwango baada ya kumfutilia kwa ukaribu nyota huyo.
Zahera alisema, mshambuliaji huyo huenda akawa hapati muda mzuri wa kupumzika kwa maana ya kulala mapema na kula chakula kizuri kinachoendana na michezo na kujikuta akicheza chini ya kiwango.
“Nimekaa na kumfanyia tathmini Makambo nimegundua mambo mawili ambayo yanafanya kiwango chake kishuke kwa haraka na muda mfupi tofauti na matarajio yangu.
“Namshamshauri afuate miiko ya soka kwa kuweka muda mzuri wa kupumzika kwa maana ya kulala, kupata lishe bora akifanya hivyo atarejea kwenye ubora wake," alisema.
Makambo amefikisha mabao matatu kwenye ligi kuu bara baada ya Kucheza michezo nane kwenye ligi kuu bara, leo wanacheza dhidi ya Lipuli Uwanja wa Taifa.
Makambo ni mchezaji wa kawaida sana,na mfumo wa yanga wa sasa si rafiki sana
ReplyDelete