October 30, 2018

Klabu ya Real Madrid imemfuta kazi kocha wake Julen Lopetegui baada ya miezi minne na nusu ya kudumu klabuni hapo.
Mhispania huyo alichukua mikoba kutoka kwa Zidedine Zidane mwezi wa sita ambapo kupoteza kwenye mchezo wa El Clasico dhidi ya Barcelona ulikuwa mchezo wa tano kufungwa katika michezo sita waliyocheza ya hivi karibuni.
Huu ni mwanzo mbaya zaidi wa Real Madrid tangu walipofanya hivyo mwaka 2001-2002.Madrid ambayo inashikilia rekodi ya kutwaa ubingwa wa klabu bingwa ulaya mara tatu,ipo nafasi ya tisa kwenye msimamo wa La Liga.
Mikoba ya Lopetegui, 52 sasa itarithiwa na kocha wa timu ya vijana ya timu hiyo, Santiago Solari ambaye amewahi kuwa mchezaji bora Madrid na kutengeneza ufalme wake.
Lopetegui alishiriki mazoezi na wachezaji siku ya Jumatatu ingawa matarajio yake yamefutwa na kikao cha dharura cha bodi ya timu hiyo kilichokaa siku ya Jumatatu jioni.
Taarifa ya klabu inasema kwamba 'Kumekuwa na utofauti mkubwa sana kati ya uwezo wa viongozi wetu (Real Madrid) na matokeo tunayoyapata mpaka sasa'.
Wachezaji wanane wa Madrid ni sehemu ya majina 30 yaliyotajwa kuwania Ballon d'Or ya mwaka 2018.Ikiwa nafasi ya tano alama tatu nyuma ya vinara Ponferradina.
Kocha mteule Solari atakumbana na ratiba rahisi ukiitazama ambapo ataanzia kwenye mchezo wa kombe la ligi ya Hispania dhidi ya timu ya daraja la nne Mellila, siku ya Jumatano.
Real itakutana Valladolid katika mchezo wa sita wa La Liga siku ya Jumamosi ambapo Novemba 7 itaikaribiana na Viktoria Plzen kwenye mashindano ya klabu bingwa Ulaya, ikifuatia mechi dhidi ya Celta Vigo.
Hii inakuwa mara ya pili kwa kocha Lopetegui kufukuzwa ndani ya mwaka mmoja baada ya kuondoshwa kwenye kikosi kilichotakiwa kusafiri kuelekea Urusi kwenye Kombe la Dunia siku mbili baada ya kugundulika amesaini mkataba wa Real Madrid.
Kutoka BBC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic