Kocha msaidizi wa timu ya Azam FC, Juma Mwambusi amesema ubovu wa viwanja mikoani unawapa tabu konyesha soka la darasani hali inayowafanya wakutane na ugumu kupata matokeo.
Mwambusi amesema kuwa wanatambua kuwa mchezo wao kesho dhidi ya Singida United utakuwa mgumu kutokana na wenyeji kupoteza mchezo wao uliopita dhidi ya Ruvu Shooting.
"Tunajua tunakutana na ushindani, viwanja vingi vya mkoani ubora wake sio wa kuridhisha hali inayofanya kuwa na ugumu, ila tunahitaji matokeo tutaonyesha mchezo wa burudani na kushinda.
"Wachezaji wetu wawili wanasumbuliwa na majeruhi wataukosa mchezo huo ikiwa ni pamoja na Agrey Moris na Joseph Mahundi, bado hawajawa sawa ila wengine wote wana morali ya kupambana kuhakikisha tunapata matokeo ugenini," alisema.
Azam wamecheza michezo 10 bila kupoteza hata mmoja wakiwa wametoa sare michezo mitatu na wameshinda michezo saba, wamejikusanyia jumala ya point 24 zinazowafanya wawe nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi Kuu Bara.
Kesho azam anapigwa mapema tu,natanguliza pole kwake na benchi LA ufundi.
ReplyDeleteKesho azam anapigwa mapema tu,natanguliza pole kwake na benchi LA ufundi.
ReplyDelete