October 27, 2018


Kocha wa Coastal Union amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao timu ya Alliance FC, licha ya kutokuwa na mwenendo mzuri kwenye ligi kwa sasa baada ya kufungwa mabao 5-1 dhidi ya Simba,wamepania kuwaongeza maumivu kwa kuondoka na pointi tatu .

Mgunda amesema kuwa ugumu wa ligi ni mkubwa kila timu anaiheshimu kwa kuwa mpira ni mchezo wa uwanjani watapambana kuhakikisha wanaweza kupata ushindi katika  mchezo huo.

"Ari ya vijana ipo vizuri kuhakikisha tunapata matokeo mazuri, hatuwezi kuwadharau alliance kwa kuwa ni timu ambayo ipo kwenye ligi, wachezaji wameniahidi kupata matokeo ili kuweza kujiimarisha nafasi ambayo tupo kwenye 'top ten'," alisema.

Coastal Union imecheza michezo 11,  imejikusanyia jumla ya pointi 15, katika michezo hiyo,  kesho watacheza dhidi ya Alliance FC kufikisha mchezo wa 12, zote ni miongoni mwa timu ambazo zimepanda daraja msimu huu.

1 COMMENTS:

  1. Habari haijakamilika watacheza kesho kwenye uwanja gani na mechi inatarajiwa kuanza saa ngapi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic