October 4, 2018


Kocha Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems anafikiria kufanya uamuzi ndani ya kikosi chake kwa kuanza kuwatumia washambuliaji ambao hawapati nafasi ya kucheza akiwemo Adam Salamba na Mohamed Rashid kwa kile alichokitaja ubutu wa kufunga mabao.

Kauli hiyo aliitoa dakika chache baada ya mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga kumalizika kwa suluhu wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo ambao kipa wa Yanga Beno Kakolanya ali­ibuka nyota wa mchezo huku Kocha Mwinyi Zahera akikiri kwamba aliwaambia wachezaji wake wapaki basi.

Huo, ni mchezo wa tatu wa ligi unamalizika kwa washam­buliaji wake tegemeo wal­iokuwepo kwenye kikosi cha kwanza Emmanuel Okwi na Meddie Kagere kutoka uwan­jani bila kufunga, mingine ni dhidi ya Ndanda FC na Mbao.

Kwa mujibu wa Championi Jumatano, Aussems alisema amesikitishwa na nafasi nne za wazi ambazo washam­buliaji wake wamezipata na kushindwa kuzitumia vema kufunga mabao katika mchezo wao na Yanga na hilo lime­tokana na umakini mdogo wa wachezaji hao, lakini ubora wa Kakolanya.

“Utafikia muda nitaanza kuwatu­mia washambuliaji ambao hawapati nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza kwa kuwa nimeona wale ambao wapo hawanipi ninachotaka,”alisema Kocha huyo ambaye ana presha kubwa kutokana na gharama ya kikosi chake na malengo aliyopewa na uongozi.

“Kwa sababu mimi nina­taka kuona washambuliaji wakifunga mabao kwa faida ya timu na siyo kitu kingine, hilo wazi kama washambuliaji wangu wamecheza mechi tatu za ligi bila ya kufunga bao hakuna sababu ya kuen­delea kuwatumia na badala yake ninatakiwa kuwatumia wengine, sawa kipa wa Yanga alikuwa bora kwa nini wao hawakuwa bora kufunga.

“Hivyo, nimepanga ku­watumia washambuliaji wengine ambao hawapati nafasi za kucheza ili na wao waonyeshe uwezo wa kufun­ga mabao, labda wanaweza kutupa matokeo mazuri,” alisema Aussems. Mpaka mchezo huo unamalizika, Simba iliongoza kwa umiliki wa mpira ambao ni 62% kwa 38% lakini mashuti ya maana yaliyolenga lango yaliyopigwa na mastraika wa Simba ni 14 wakati Yanga ni matatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic