October 9, 2018


Nyota ya Mtanzania, Mbwana Ally Samatta anayekipiga katika klabu ya KRC Genk huko Ubelgiji imezidi kung'aa baada ya kuanza kuwaniwa na vilabu vikubwa barani Ulaya.

Taarifa ambazo zipo mitandaoni hivi sasa kutoka vyanzo kadhaa huko England zinaeleza kuwa nyota huyo anawaniwa na klabu tatu zinashoriki ligi kuu England.

West Ham, Everton na Burnely zimetajwa kuanza kumvutia waya Samatta ambaye amekuwa tegemeo ndani ya klabu yake.

Samatta ameingia kwenye vichwa vya habari England ikiwa ni wiki kadhaa zimepita tangu aanze kuhusishwa kutimkia Spain katika timu baadhi zinazoshiriki Ligi Kuu 'La Liga'

Mchezaji huyo hivi sasa yupo hapa nchini tayari kuelekea Cape Verde kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kuelekea AFCON 2019 na kikosi cha Taifa Stars.

2 COMMENTS:

  1. Kabisa nyota njema inazidi kumuwakia vyema Samata na M/Mungu ampe uwezo zaidi na amkinge hasada Amen. Tetesi zinasema kama Samata ataendeleza moto wake wa kufunga magoli katika kipindi hiki basi vilabu vikubwa kadhaa vinatarajiwa kuingia katika vita ya kuinasa saini yake. Hii inamaana kubwa sana kwa Samata na wachezaji wa timu ya Taifa Stars. Samata anafuatiliwa kwa karibu sana na team nyingi barani ulaya inaana hata hii mechi ya Cape Verde ya kufuzu Afcon kutakuwa na maskauti wengi watakaokuwa wanamfuatilia Samata lakini ni nafasi pekee kwa wachezaji wengine hasa wa Stars kuonesha uwezo wao huwezi kujua nani anafuatilia. Katika mechi ya Cape Verde kama ujumbe utafika wachezaji wa taifa stars wanatakiwa kufanya mambo matatu.(1) kujua yakwamba kiongozi wao ambae ni kapteni wa timu ya Taifa Mbwana Samata anahitaji msaada japokuwa hawezi kuwatamkia hadharani kuwa anahitaji msaada,lakini anahitaji msaada wa kuhakikisha taifa stars inacheza vizuri na kushinda katika mechi hiyo na Mungu ajalie Samata azidi kuonesha uwezo wake wa kufunga magoli zaidi. Haitakuwa kazi rahisi mbele ya Cape Verde ila ndipo pale tunaposema wachezji wa Stars wanatakiwa kujiandaa kwa jihadi katika mechi hiyo ili kujijengea mazingira mazuri zaidi ya kufuzu.(2) jambo la pili wanalotakiwa kufanya wachezaji wa taifa stars ni kujiamini na kufahamu yakuwa mechi ya mpira hachezwi siku nzima ila nasa moja na nusu na mapumziko ndani yake, ndani ya masaa 24 yanayokamilisha siku. Kwa hivyo kuna masaa 23 na nusu ya kupumzika baada ya kazi ya lisaa limoja na nusu kwa hivyo mchezaji atakaepata nafasi ya kuliwakilisha taifa awe tayari wa kujitoa kwa kila dakika ya mchezo kiakili na kimwili bila ya kufikiria fulani anafanya nini,mchezaji anatakiwa kujigalia yeye mwenyewe binafsi kwanza anaifanyia nini timu ili kuhakisha inapata ushindi kabla ya kufikiria fulani atafanya, Timu ni wachezaji bila ya kuwa na uweledi wa mchezaji mmoja mmoja kutambua uzembe au kushindwa kwake kutimiza majukumu yake kikamilifu huwa mara nyingi ndio anguko na timu zima .(3) Nidhamu katika mchezo na kufuata maelekezo ya kocha na kutumia uwezo wao binafsi katika kuipigania timu. Vile vile ushirikiano hasa katika finishing kwa wachezaji wa mbele au washambiaji katika kufanaya maamuzi sahihi wakati wanapolikaribia goli ni jambo la msingi sana. Golini ni sehemu ya pressure ila hata katika tendo la ndoa mwanamume mwenye utulivu asiekuwa na papara basi anafasi kubwa zaidi ya kumridhirizisha mpenziwe. Kwa kawaida kama fowadi alielikaribia goli anaetaka kufunga akibanwa lazima kutakuwa na wachezaji wenzake ambao wapo free ni wakati wa fowadi aliebanwa kuwa na maamuzi ya haraka ya kutishia kufunga huku macho yake yakiangalia goalkeeper au goli kakini miguu yake ikiangaza mchezaji mwenzake aliekuwa kwenye nafasi sahihi na kumpasia.Sio kitu rahisi kama tunavyozungumza lakini watanzania sisi ni watu majasiri wa kiakili na kimwili tukiamua ila tunashindwa kujielewa siku ikifika kujitambua basi hakuna misri wala Nigeria.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic