October 30, 2018

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 33, amesema aliihama Real Madrid na kujiunga na Juventus kwa sababu rais wa klabu hiyo ya Uhispania Florentino Perez hakumfanya ajihisi kama mchezaji anayethaminiwa na kudhaminiwa sana. (L'Equipe, kupitia Express).
Real Madrid wanamtaka meneja wa sasa wa Tottenham Mauricio Pochettino awe meneja wao mpya wa kudumu kufikia mwisho wa mwezi huu. Miamba hao wa Uhispania walimfuta kazi Julen Lopetegui baada yake kuhudumu kwa miezi minne na nusu Jumatatu. Alifutwa baada ya Madrid kuchapwa 5-1 na Barcelona Jumapili. (Sun).
Besiktas wanataka kumrejesha kipa wa Liverpool Loris Karius kwa klabu hiyo ya Anfield. Kocha huyo alitia saini mkataba wa mkopo wa miaka miwili na klabu hiyo ya Uturuki.
Meneja Jose Mourinho ataungwa mkono Januari kuwanunua wachezaji zaidi kuimarisha kikosi cha Manchester United iwapo atawapata wachezaji wafaao. Inadaiwa kwamba ametengewa kitita cha karibu £100m. (Guardian).
Mwanawe Vichai Srivaddhanaprabha, Aiyawatt, aliyekuwa wa kwanza kumhoji meneja Claudio Ranieri aliyewasaidia kushinda Ligi Kuu ya England kabla yake kuteuliwa rasmi, anatarajiwa kuongoza Leicester baada ya babake kufariki katika ajali ya helikopta iliyoua babake na watu wengine wanne. (Mail).
Mshambuliaji wa Barcelona anayechezea Ufaransa Ousmane Dembele huenda akaruhusiwa kuondoka klabu hiyo mwezi Januari. Chelsea, Liverpool na Arsenal ni miongoni mwa klabu ambazo zimehusishwa na kutaka kumchukua mchezaji huyo mwenye miaka 21. (Sun).
Juventus wanataka sana kumnunua beki wa miaka 21 kutoka Serbia Nikola Milenkovic, ambaye anadaiwa pia kunyatiwa na Tottenham na Manchester United. Juve pia wanamtaka kiungo wa kati wa Italia Federico Chiesa, 21, lakini Fiorentina huenda wakataka kulipwa zaidi ya euro 100m (£89m) ndipo wakubali kuwaachilia wawili hao. (Calciomercato).

    Meneja wa zamani wa Aston Villa Steve Bruce anahusishwa na kuhamia Reading. Klabu hiyo kwa sasa inashikilia nafasi ya 22 kwenye ligI ya wakiwa na Paul Clement. (Birmingham Mail).
    Meneja wa Bournemouth Eddie Howe amemhakikishia mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya England Jermain Defoe kwamba bado anahitajika Bournemouth, licha ya mshambuliaji huyo mwenye miaka 36 kuchezeshwa mara tatu pekee Ligi ya Premia, wakati wote akiingia kama nguvu mpya. (Mirror).
    Manchester United hawajawasiliana na mkurugenzi wa michezo wa RB Leipzig Paul Mitchell kuhusu kuhudumu katika nafasi kama hiyo ambayo wanapanga kuianzisha Old Trafford. Hata hivyo, mkuu huyo wa zamani wa usajili wa wachezaji Tottenham anafurahia kuhusishwa na kazi hiyo. (Sun).
    Kiungo wa kati wa Liverpool kutoka Brazil Fabinho, 25, anasema amekumbwa na matatizo katika kujaribu kuzoea maisha mapya tangu alipohamia Anfield kutoka Monaco kwa £39m majira ya joto. (ESPN).
    Kutoka BBC

    1 COMMENTS:

    TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

    GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

    B2.jpg
    Image and video hosting by TinyPic