October 15, 2018


KOTEI


Kiungo wa Simba, James Kotei atakosa mechi tatu za Ligi Kuu Bara kutokana na kosa la kumpiga Gadiel Michael wa Yanga.


Adhabu hiyo imetolewa na kamati ya nidhamu TFF  kupitia Kanuni ya 38 ya kifungu cha tatu udhibiri wa wachezaji.


Pamoja na hivyo, Kotei anakutana na adhabu ya kulipa faini ya Sh milioni moja.

DANTE


Pamoja na Kotei, mwingine anayekutana na adhabu hiyo ni beki wa Yanga,Andrew Vicent maarufu kama Dante ambaye alijaribu kumpiga kichwa nahodha wa Simba, Mohamed Zimbwe ‘Tshabalala’.

Matukio yote mawili. yalitokea wakati wa mechi ya watani, Simba na Yanga ambayo ilimalizika kwa sare ya bila kufungana.


5 COMMENTS:

  1. Eti alijaribu kumpigia kichwa.Acheni mapenzi kosa limeonekana na kapewa adhabu sawa na Kotei.Hivyo mliremba eti mpira ulimpiga mkononi Tambwe mpaka hivi karibuni kakiri kwamba alishika na refa hakumwona.Pendeni lakini ripotini haki.

    ReplyDelete
  2. Vizuri haoYanga ndio wakome kufukunyua baadhi ya mambo kwani walidhani wataikomoa Simba kumbe.teh teh teh wacha nicheke.

    ReplyDelete
  3. Ukifanya kosa unaadhibiwa haijalishi ni aina gani la kosa,hivyo mashabiki acheni kuwapangia Tafuna Fedha Fasta cha kufanya.Kama hujaridhika kata rufaa,ila inatia aibu kwa mchezaji wa kulipwa toka Zaidi ya maili 6588 hadi Tanzania kufanya upuuzi ule,shame on him!

    ReplyDelete
  4. Kufanya kosa haijalishi unatoka wapi.Uwe wa Mvomero au wa Jamaica ukifanya kosa unaadhibiwa .Ndio maana Dante när kafungiwa .Mchezaji wa kulipwa!!!!Kwani Dante mchezaji wa bure? UKICHIMBA SHIMO USIKIREFUSHE KWANI INAWEZAKANA NA WEWE UKADUMBUKIA. UHASIDI HAUJAWAHI KUMUACHA MTU SALAMA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic