October 15, 2018





Mshambuliaji Mtanzania wa KRC Genk, Mbwana Samatta anatamani sana kucheza nchini England na ndiyo ndoto yake.

Hayo yamesemwa na meneja wake, Jamal Kisongo ambaye amesema Samatta amekuwa akipambana na siku moja atafikia hivyo.

“Kweli hii ni ndoto yake anatamani sana kucheza nchini England. Lakini ni suala la kufuata utaratibu na wakati, ndiyo maana unaona anapambana vilivyo.

“Haya mambo hayawezi kupatikana tu ili mradi, yanahitaji juhudi na maarifa ili kuyafikia. Kama unavyoona, Samatta anapambana vilivyo kufikia hapo,” alisema.

Hivi karibuni, timu zinazoshiriki Ligi Kuu England, Everton ikiwa moja wapo, zimeonyesha kuvutiwa na kiwango cha Samatta ambaye ndani ya mwezi mmoja alifunga hat trick mara mbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic