October 28, 2018



Baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga, Obrey Chirwa aliondoka na kujiunga na klabu ya Nogotoom ya nchini Misri ,inadaiwa amevunja mkataba kutokana na kushindwa kulipwa stahiki zake, hivi karibuni alikuwepo uwanjani kushuhudia Yanga wakicheza na Alliance FC.

Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa kutokana na kocha Mkuu Mwinyi, Zahera kutomkubali walikaa naye kikao cha dharula kwa muda wa siku mbili wakimtaka akubali mshambuliaji huyo asajiliwe.

"Suala la Chirwa kurudi Yanga linaonekana kuwa mada kubwa ndani ya uongozi hasa kupitia kamati ya usajili ile ya mashindano, wamefuata masharti ili wamrejeshe Chirwa,  wanakwama kutokana na misimamo ya Zahera hali iliyopeleka wakae kikao ili kocha amsamehe Chirwa.

"Kocha alitoa masharti kwamba Chirwa mwenyewe inabidi aitwe kwenye kikao ili aombe radhi kwa yale aliyofanya kwa kocha kabla ya kuondoka na kamati kuhakikisha inasimamia nidhamu yake," kilieleza chanzo.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema kuwa hakuna kiogozi aliyeonana naye zaidi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili (Hussein Nyika) na Makamu (Mustafa Olungu) kuzungumzia suala la Chirwa, walinipongeza kwa ajili ya misimamo yangu ya kutomkubali Chirwa.

"Nilichukizwa na kitendo cha mtu kutoka ndani ya timu ambaye alimtumia tiketi Chirwa ili aje kujiunga na Yanga bila mimi kujua, kuna mtu alianza kumshawishi Nyika na Olungu wakubali, nilipokataa walinifafanulia vizuri kwa hiyo sasa nimenyamaza na kuwasikiliza watakachoafikiana wao nipo tayari," alisema.

Chirwa alidumu kwa misimu miwili ndani ya Yanga, aliondoka msimu uliopita akiwa amefunga mabao 12, iliwahi kuripotiwa kuwa aligoma kuichezea timu hiyo akishinikiza alipwe fedha zake wakati huo Yanga ilikuwa kwenye hali mbaya kiuchumi.

7 COMMENTS:

  1. Ndio timu zetu. Kiongozi anamleta mchezaji bila mawasiliano na kocha .Mchezaji wa aina hiyo lazima awe msumbufu sababu anajua kuna mtu anachukua 10%. Lakini timu ikifanya vibaya lawama kwa kocha

    ReplyDelete
  2. Kwanza hajui kupiga penati pili hafai kuchezea ligi kuu labda mumupeleke ligi daraja LA kwanza akakuze kiwango ligi kuu atapata tabu xana

    ReplyDelete
  3. Kwanza hajui kupiga penati pili hafai kuchezea ligi kuu labda mumupeleke ligi daraja LA kwanza akakuze kiwango ligi kuu atapata tabu xana

    ReplyDelete
  4. Wanini hiyo?Alisha itia Yanga hasara hiyo.Akaenda kulima matikiti kwao,wakati Yanga inasota.aliporudi akadai mshahara wake ambao hakufanyia kazi.Yanga ilimlipa.kisha akachomoka.Waninu hiyo MTU hats taiga lake halimwiti kuchezaa nchi.Nampongeza Zahera Kwa uamuzi wake.Hao viongozi Wa Yanga wameshaanza upuuzi wao Wa kuwaleta wachezaji wenye misimamo ya kukatwa 10%.
    Tunamtaka Zahera wetu.Kama mchezaji anajielewa kuwa anayo nguvu ya viongozi basis hudharau makocha.Zahera analijua hill.Kaza Uzi Mzee.Aondoke hiyo Kijana,abakie Zahara wetu.

    ReplyDelete
  5. Mtoto akinyea kiganja cha mkono utakikata?Wampe nafasi tena Chirwa yaweza kuwa amejifunza kitu.Kiukweli bado ni mshambuliaji mzuri kuliko huyo makambo aliyemleta Zahera,Kitu gani kitatuaminisha kama hao washambuliaji anaosema ni Matata wanaweza wakawa wa kawaida sana angalia alivyomleta kipa wake KINDOKI

    ReplyDelete
  6. Huyo kocha aende zake asitake kutujazia wacheza sebene kwenye timu yetu maana anawataka wakongo tu. Chirwa katoka Zambia kaja kutafuta maisha. Hawezi kaa miezi bila kulipwa then utoe jasho tu uwanjani wakati watoto wanakufa njaa. Kindoki kaletwa anafanya nn hapo? Makambo naye legelege kama mcheza sebene. Eti anamtaman kagere huo si uchizi. Chirwa ni mpambanaji kuliko hayo matakataka ya Kongo

    ReplyDelete
  7. Huyo kocha aende zake asitake kutujazia wacheza sebene kwenye timu yetu maana anawataka wakongo tu. Chirwa katoka Zambia kaja kutafuta maisha. Hawezi kaa miezi bila kulipwa then utoe jasho tu uwanjani wakati watoto wanakufa njaa. Kindoki kaletwa anafanya nn hapo? Makambo naye legelege kama mcheza sebene. Eti anamtaman kagere huo si uchizi. Chirwa ni mpambanaji kuliko hayo matakataka ya Kongo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic