Katika michezo mitatu iliyopita Aussems amefanikiwa kuvuna pointi tisa na kushinda mabao 10, amefungwa mabao 2 pekee yupo nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia pointi 20 nyuma ya Yanga yenye pointi 22 kinara ni Azam akiwa na pointi 24
"Jambo ni moja tu ndio lipo mbele yetu na siyo lingine zaidi ushindi, tunataka kukusanya pointi nyingi katika michezo yetu tunajua mechi itakuwa ngumu lakini pointi tatu ndiyo kitu muhimu tunachokitaka.
Katika michezo nane ambayo Ruvu wamekutana na Simba tangu msimu wa 2013/14, Simba imeshinda michezo saba na wamelazimisha sare moja tu kwa mechi ambayo ilichezwa mchana na siyo usiku kama leo Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment