Timu ya Tifa ya Tanzania ya Beach Soccer inayoshiriki mashindano ya Fainali za Kombe la Mataifa kwa Afrika (Afcon) imepangwa kundi B katika droo iliyofanyika nchini Misri yanatarajiwa kuanza Desemba 8-14 nchini Misri.
Tanzania ambayo ipo chini ya Kocha Boniphace Pawasa, liipata nafasi ya kushiriki mashindano hayo baada ya timu Afrika Kusini kujitoa kwenye mashindano hayo katika hatua za awali .
Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) Cliford Ndimbo amesema kuwa Tanzania itakuwa kundi moja pamoja na timu za Senegal, Nigeria na Libya.
Kundi A lina timu kama Misri, Morocco, Ivory Coast na Madagscar.
0 COMMENTS:
Post a Comment