Ofisa wa habari wa timu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa wapo tayari kuchukua pointi tatu muhimu katika mchezo wao wa leo dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa Uwanja wa Taifa saa 1:00
Manara amesema kuwa wachezaji wana morali katika kutafuta matokeo hivo wanaamini watafanya vizuri kutokana na mfumo ambao umetambulishwa na Kocha Mkuu Patrick Aussems.
"Tunataka matokeo kuendelea kutetea ubingwa wetu licha ya kucheza tunawafurahisha pia mashabiki tumejiandaa vizuri ili kupigania nafasi za juu tunacheza na kutoa burudani.
"Unaweza kushinda na ukacheza huku unaumwa, sisi tunashinda na mashabiki wanafurahia wapinzani wetu ni timu nzuri huwezi kuidharau timu ambayo ipo ligi kuu, wachezaji wanajua kazi yao hasa wakiwa uwanjani tunahitaji pointi tatu hata tukiwa nyumbani wao pia wanahitaji pointi tatu pia," alisema.
Mchezo wa kwanza msimu uliopita uliowakutanisha Simba na Ruvu Shooting, Ruvu walipoteza kwa kufungwa mabao 7-0 huku Emmanueli Okwi akifanikiwa kufunga mabao 4.
0 COMMENTS:
Post a Comment