October 10, 2018






Uongozi wa Singida United na klabu ya Mamelod Sundowns uko kwenye hatua za mwisho  kuweza kufikia makubaliano ya kumuuza nyota wa Singida United Habibu Kyombo, aliyefanikiwa kufuzu majaribio kwenye klabu hiyo.


 Kyombo alikwenda kufanya majaribio katika klabu ya Mamelod mapema Agosti 20, mwaka huu, kwa muda wa siku kumi na baadaye waliweza kumuongezea siku nyingine zaidi kuweza kumuangalia na sasa inaelezwa kuwa ameshafuzu.

  Taarifa za ndani kutoka ndani ya klabu hiyo zinadai kuwa  tayari mambo yanaenda vizuri kwa klabu hizo mbili na wakati wowote Kyombo anaweza kuondoka na kujiunga na klabu yake hiyo mpya.

“Kyombo mambo yake tunaweza kusema kwa upande mwingine yapo hatua za mwisho kabisa, ni asilimia 90, bado 10 tu. Sababu timu zimeshakubaliana kwa asilimia kubwa kilichobaki ni kidogo na dili likikamilika tu anaweza kuondoka muda wowote na kujiunga na klabu yake mpya  ya Mamelod ambapo alifanikiwa kufuzu majaribio,” kilisema chanzo.

 Kwa upande mwingine kinda mwingine wa kikosi hicho, Ally Ng’azi ambaye ni zao la Serengeti Boys amefanikiwa kupata klabu moja katika Jamhuri ya Czech ambayo ataenda kuitumikia moja kwa moja timu hiyo.

1 COMMENTS:

  1. Kama hujamuona Kyombo na uzi wa mamelod basi usiamini chochote hizo ni blah blah za kawaida na zilishatokea kwa wachezaji kadhaa ila hakuna kilichoendelea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic