October 11, 2018


Klabu ya Real Madrid imeanza kummendea mshambuliaji wa Manchester City na England Raheem Sterling, 23, baada ya mshambuliaji huyo kubakiza miaka miwili kwenye mkataba wake. (ESPN)

Liverpool na Manchester United zimeanza kupigana vikumbo kumuwania kiungo mshambulaiji wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 27.(London Evening Standard)

Pamoja na hivyo vilabu hivyo vitakumbwa na upinzani kutoka Turin Juventus. (Mail)

Manchester United imeanza mpango wakufanya mazungumzo ya awali na beki wa Barcelona na Jordi Alba, 29. (Mundo Deportivo, via Mirror)

United ipo katika mchakato wa mazungumzo ya mkataba mpya kwa mshambulaiji wao Jesse Lingard, 25, wiki ijayo. (Metro)

Arsenal na United zitakutana na ushindani kutoka Bayern Munich katika kumshawishi winga wa Lille na Ivory Coast Nicolas Pepe, 23. (Bild, via Talksport)

Klabu ya AC Milan imezishinda mbio vilabu vya Liverpool na United kumsainisha kinda wa wa Flamengo na Brazil, Lucas Paqueta,21. (Sun)

Kiungo wa Liverpool na England Adam Lallana, 30, atarejea kujiunga na klabu yake baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa. (Times - subscription required)

Beki wa kushoto wa Hispania Marcos Alonso, 27, amesema yuko njia panda kama aongeze mkataba Chelsea. (Mirror)


Klabu ya Chelsea inaweza ikatupa karata yake kushindana na Manchester United katika kupata saini ya beki wa AC Milan na Italia Alessio Romagnoli, 23. (Sun)

Winga wa Liverpool na Uswiswi Xherdan Shaqiri, 27, amesema hajatembelea bado makao makuu ya England tangu amejiunga na Liverpool msimu huu. (Blick, via Mail)

Mshambualiaji wa Leicester Jamie Vardy, 31, na mke wake wamepanga kufuata nyanyo za Winston Churchill na Dalai Lama kwa kwenda kutembelea na kufanya mazungumzo na Oxford Union. (Sun)

Watazamaji wa ligi kuu England msimu ujao kwenye mtandao wa Amazon wataweza kutazama mechi mbalimbali kwa kuchagua mtangazaji na mchambuzi mfano unaweza kuchagua wote wawe wakike. (Times - subscription required)


Chelsea wamepanga kuwapeleka mashabiki wao Auschwitz kupata elimu ya namna ya kushangilia katika uwanja wao wa Stamford Bridge bila kuleta vurugu ili kupunguza vifungo ambavyo timu hiyo inakumbana navyo. (Sun)

Kutoka BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic