Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa mtangazaji wa habari za Michezo na burudani wa Idhaa ya Kiswahili DW Isaac Gamba.
"Rais Magufuli ameshindwa kufika katika msiba kutokana na kubanwa na shughuli za kikazi hali iliyomfanya ashindwe kufika ila ametuma salamu zake za rambirambi kwa wafiwa," alisema.
Gamba alikutwa amefariki dunia akiwa nyumbani kwake mjini Bonn, Oktoba 18, ameagwa leo katika hospitali ya Jeshi ya Lugalo jijini Dar es Salaam, baada ya kuagwa mwili ulipelekwa Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kwa ajili ya kusafirishwa mpaka Mwanza na kisha kupelekwa Bunda, Serengeti, Mkoani Mara kwa ajili ya Mazishi.
Gamba alijiunga na DW mnamo mwaka 2015 akitokea Radio One ya Dar es Salaam, pia alifanya kazi Radio Free Afrika na Radio Uhuru, kwa muda mfupi alifanikiwa kufahamika kutokana na ucheshi wake na wepesi wa kufahamiana na watu.
Waliohudhuria ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkurugenzi wa Global Group Eric Shigongo,Ofisa habari wa Simba Haji Manara, rafiki wa marehemu na mfanyakazi wa DW Sudi Mnette.
0 COMMENTS:
Post a Comment