Timu ya Lipuli itashuka dimbani leo kuchezan dhidi ya Yanga katika mwendelezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Taifa.
Kocha wa Lipuli Selemn Matola amesema kuwa wamejiandaa kiasi cha kutosha kuweza kuleta ushindani katika mchezo huo kwa kuwa ana uzoefu na ligi ila atawakosa wachezaji wake muhimu watatu wa kikosi cha kwanza.
"Wachezaji wana morali ya kupamambana ila nitawakosa wachezaji wa kikosi cha kwanza ambao ni Maalim Busungu, huyu hajaniaga na sijui yupo wapi mpaka sasa, Jamali Mnyate aliumia katika mchezo wetu uliopita dhidi ya Mbao na Fred Mtwala.
"Tupo tayari kwa mapambano tutaleta ushindani dhidi ya wapinzani wetu kuhakikisha tunachukua point tatu muhimu," alisema.
Msimu uliopita Lipuli walifanikiwa kulazimisha sare dhidi ya Yanga katika mchezo wao wa kwanza na wakafungwa mabao mawili katika mchezo wa pili uliochezwa Uwanja wa Samora.
Tunawaombea kila la kheri lipuli fc wanapaluhengo
ReplyDelete