October 29, 2018

Uongozi wa timu ya Yanga umetoa tahadhari kwa wapinzani wao Lipuli FC ya kutoka mkoani Iringa ambao watacheza nao kesho katika Uwanja wa Taifa mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hussen Nyika amesema kuwa ukubwa wa kikosi cha Yanga unapaswa uheshimiwe na wapinzani kwakuwa kikosi kimejipanga kuhakikisha wanapata pointi tatu.

"Timu yetu ni kubwa, ina uwezo mkubwa wa kushindana hasa kutokana na aina ya wachezaji walio na mbinu ambazo wanapewa, tunaiheshimu Lipuli ila tutahakikisha tunapata matokeo katika mchezo wetu ambao tutakuwa nyumbani," alisema.

Yanga wamecheza michezo nane mpaka sasa kwenye ligi kuu, yote wamecheza katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kesho watakuwa na kibarua cha kucheza na Lipuli FC iliyo chini ya Selemani Matola.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic