Mchezo uliokuwa unatazamwa zaidi ni kati ya Liverpool dhidi ya Cardiff city ambapo majogoo wa jiji la Liverpool imeibuka na ushindi wa mabao 4-1.
Magoli ya liverpool yamefungwa na Sadio Mane 2, Mohamed Salah 1, na Shaqiri amefunga goli 1.
Ushindi wa Liverpool unaipeleka timu hiyo kileleni mwa msimu kwa kujikusanyia alama 26 juu ya Manchester City ambayo ina alama 23 na itakuwa na mchezo siku ya Jumatatu dhidi ya Tottenham Hotspurs.
Matokeo ya michezo mingine
- Watford wameshinda goli 3-0 dhidi ya Huddersfield Town.
- Fulham wakapata kipigo cha 3-0 dhidi ya AFC Bournemouth.
- Southampton wamekutana na wabishi Newcastle United na kutoshana nguvu ya kutofungana.
- Brighton & Hove Albion imeshinda goli 1-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers.
Kutoka BBC.
0 COMMENTS:
Post a Comment