October 28, 2018


Baada ya kupoteza michezo yao miwili kanda ya ziwa , Uongozi wa Mtibwa Sugar umekaa kikao na wachezaji wake ili  kujua kinachowasumbua kwenye michezo yao, leo watacheza na Kagera Sugar Uwanja wa Manungu.

Ofisa habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema walipoteza michezo yao miwili mfululizo dhidi ya Mbao kwa kufungwa bao 1-0, wakapoteza dhidi ya Stand United kwa kufungwa mabao 2-1.

"Tumekaa na wachezaji kwa muda wa masaa matatu ili kuzungumza nao kwa ukaribu, wametuambia kinachowasumbua, hivyo wametuahidi kuonyesha maajabu katika mchezo wetu wa leo dhidi ya Kagera Sugar, mashabiki waendelee kutupa sapoti," alisema.

Mtibwa Sugar watakutana na Kagera Sugar ambayo  haijapoteza mchezo hata mmoja kwenye ligi baada ya kucheza michezo 10, wanashika nafasi ya 8 wakiwa na pointi 16, Mtibwa wamekusanya pointi 17 wanashika nafasi ya 4 baada ya kucheza michezo 11.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic